Wednesday, September 10, 2014

#Wakristo na jamii kwa ujumla wametakiwa kuwa na ushirikiano na kujenga tabia ya kumtolea Mungu kwa uaminifu.

Wito huo umetolewa na askofu mkuu wa kanisa la Free Pentecoste Church of Tanzania FPCT David Batenzi kataika Mkutano Mkuu wa tano wa FPCT ulionza hii leo mjini Dodoma ambapo maaskofu,wachungaji na wakuu wa idara zote za kanisa hilo wamehudhuria.

Mkutano huo unatarajiwa kuhitimishwa na uchaguzi mkuu wa viongozi wa Kitaifa wa FPCT kwa ngazi ya askofu mkuu,makamu askofu,katibu mkuu,naibu katibu mkuu na afisa utawala tarehe kumi na nne siku ya jumapili pamoja na kuwekwa wakfu viongozi watakaochaguliwa.

Kwa upande wao wajumbe wa mkutano huo wameshauri mawimbi ya habari maalum Fm yafike mbali zaidi na kusisitiza juu ya maazimio ya kikao kilichopita kilichofanyika mwezi wa saba mwaka huu ambapo kila jimbo la FPCT lilitakiwa kununua kifaa maalum kwa ajili ya kufanikisha suala hilo....

No comments:

Post a Comment