MWANADAMU
HAKUPOTEZA DINI BALI ALIPOTEZA UFALME WA
MUNGU
DR.
MYLES MUNROE alihubiri kupinga dini
katika makanisa ya leo
Yeye
alikua na dini ya baba yake ambayo haikumfikisha popote katika huduma yake
Siku
moja alimuuliza baba yake kuhusiana na dini yao baba yake akamwambia dini ndio
kila kitu ila Dr.Myles Munroe akamwambia baba yake kwamba dini haitufikishi
popote na leo hii Dr.Myles anakanisa
kubwa nchini kwao na baba yake anakaa mstari wa mbele kabisa. Hivyo dini
haitupeleki popote bali imani na wokovu wa kweli.
DR.MYLES MUNROE
DR.MYLES MUNROE ......Aliongelea swala zima la kwenda mbinguni
Akasema
sisi tunataka kwenda mbinguni na wachungaji wetu wanatufundisha kuhusu kwenda
mbinguni na kumbe muda bado wa kwenda mbinguni.
Tunatakiwa kufanya kazi kabla ya kuwaza kwenda mbinguni Mungu anatuombea tubaki duniani na sisi
tunaomba kwenda mbinguni. Tufanye kazi ya kubadili dunia kabla ya kwenda
mbinguni.
Tunataka
mabadiliko serikalini wakati wachungaji hawataki watu kuingia kwenye siasa,
michezo,uchumi wa nchi....Sisi ni chumvi ya ulimwengu lazima tufanye mabadiliko
katika nchi
Mf. Dr.Myles
nchini kwao hawafanyi maamuzi
bila kumuuliza yeye
Kupitisha
sheria ya ndoa ya jinsia moja walimuuliza kama inafaa nae akawaambia haifai na
mpaka sasa hakuna ushoga wala ndoa ya jinsia moja nchini kwao.
Kila mchungaji aliye kuwepo alipata massage yake
nakujiona wapi alikua amekwenda kinyume
Mchungaji Mwakibolwa nae alikuwepo
Pastor Safari nae alikuwepo.
Mama Rwakatare alisema asante Mungu kwa message hii kwa
maana yeye alipigwa vita ya kuwa mwanasiasa wakati yeye ni mchungaji akasema
yeye ni mfanyabiashara, mwanasiasa na mjasiriamali akasema anashule kumi na
nane nchini, anafundisha ujasiriamali kanisani kwake na pia ni mbunge.
Aliwakaribisha waliookoka kwenye siasa kwa mwaka 2015.
Mr & Mrs Dr.Myles Munroe
Mchungaji Huruma Nkone nae alikuwepo.
Dr.Myles Munroe alisaini vitabu vilivyonunuliwa siku
hiyo
Viongozi na wachungaji mbalimbali walipata picha ya
ukumbusho na Dr.Myles Munroe