Thursday, October 23, 2014



MWANADAMU HAKUPOTEZA DINI BALI ALIPOTEZA UFALME  WA MUNGU­­

DR. MYLES MUNROE  alihubiri kupinga dini katika makanisa ya leo
Yeye alikua na dini ya baba yake ambayo haikumfikisha popote katika huduma yake
Siku moja alimuuliza baba yake kuhusiana na dini yao baba yake akamwambia dini ndio kila kitu ila Dr.Myles Munroe akamwambia baba yake kwamba dini haitufikishi popote  na leo hii Dr.Myles anakanisa kubwa nchini kwao na baba yake anakaa mstari wa mbele kabisa. Hivyo dini haitupeleki popote bali imani na wokovu wa kweli.



                                                                 DR.MYLES MUNROE


DR.MYLES MUNROE      ......Aliongelea swala zima la kwenda mbinguni
Akasema sisi tunataka kwenda mbinguni na wachungaji wetu wanatufundisha kuhusu kwenda mbinguni na kumbe muda bado wa kwenda mbinguni.  Tunatakiwa kufanya kazi kabla ya kuwaza kwenda mbinguni  Mungu anatuombea tubaki duniani na sisi tunaomba kwenda mbinguni. Tufanye kazi ya kubadili dunia kabla ya kwenda mbinguni.
Tunataka mabadiliko serikalini wakati wachungaji hawataki watu kuingia kwenye siasa, michezo,uchumi wa nchi....Sisi ni chumvi ya ulimwengu lazima tufanye mabadiliko katika nchi
Mf.  Dr.Myles   nchini kwao hawafanyi maamuzi bila kumuuliza yeye
Kupitisha sheria ya ndoa ya jinsia moja walimuuliza kama inafaa nae akawaambia haifai na mpaka sasa hakuna ushoga wala ndoa ya jinsia moja nchini kwao.



     Kila mchungaji aliye kuwepo alipata massage yake nakujiona wapi alikua amekwenda kinyume


                                                Mchungaji Mwakibolwa nae alikuwepo
                                                                                                           Pastor Safari nae alikuwepo.


Mama Rwakatare alisema asante Mungu kwa message hii kwa maana yeye alipigwa vita ya kuwa mwanasiasa wakati yeye ni mchungaji akasema yeye ni mfanyabiashara, mwanasiasa na mjasiriamali akasema anashule kumi na nane nchini, anafundisha ujasiriamali kanisani kwake na pia ni mbunge. Aliwakaribisha waliookoka kwenye siasa kwa mwaka 2015.


                                                                                        Mr & Mrs Dr.Myles Munroe



                                                                                   Mchungaji Huruma Nkone nae alikuwepo.




                                          Dr.Myles Munroe alisaini vitabu vilivyonunuliwa siku hiyo



          Viongozi na wachungaji mbalimbali walipata picha ya ukumbusho na Dr.Myles Munroe



No comments:

Post a Comment